Unaye mama wewe!

Joseph Wresinski, aliyeanzisha Shirika la kimataifa ATD Dunia ya Nne, alizaliwa na kukua katika familia maskini kuzidi kiasi. Alijua kukosa fedha, kuteseka, kudhalilishwa… Katika sehemu inayofuata anatuambia jinsi mama yake alivyowafundisha watoto wake kujivunia.

Kwa kweli nilikuwa mtoto mtukutu kabisa katika mazingira yote ya jirani na daima nilikuwa katika matatizo ya kila namna. (…) Jirani zangu hawakupendezwa kabisa na tabia yangu na wakati mwingine nilimsababishia mama yangu matatizo makubwa sana. Mama alihofia sana kuhusu sifa njema ya familia, hivyo watu walimshauri aniweke katika nyumba ya yatima. Kila mtu alipendekeza hivyo. Kisha usiku ule kabla sijaondoka, mama alisema, “Hapana, haiwezekani, wewe si yatima, unaye mama wewe!” Hakika mama yangu ndiye aliyenisababisha nijihusishe na familia zinazoishi katika wimbi la umaskini. Baba yangu aliondoka nyumbani kwenda kutafuta kazi, hivyo mama yangu alibaki peke yake akiwa na watoto wanne.. hata hivyo tunamshukuru mama kwamba hatukuwa na majonzi ingawa mara kwa mara tulidhalilishwa, lakini mara zote mama alifahamu jinsi ya kutufanya tujisikie vizuri tena. Tunamshukuru kwamba kwa jinsi hiyo tulikuwa na utambulisho, kwamba tulikuwa watu fulani katika mazingira ya jirani.

Hata katika hali ya ufukara wake, mama daima kwa namna moja ama nyingine alipata msaada kwa sababu alilinda heshima yake na kujivunia hali yake. Daima alitufundisha kuwa na fahari katika hali yetu. Endapo mtu yeyote alionesha hali ya kutudharau, mama alimkemea akisema, “kamwe sikubaliani na hilo.” Kwa jinsi hiyo, watu walituheshimu.

0 comments Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.