“Wajibu wa kimaadili na kisiasa na msimamo wa kisayansi unalazimisha Chuo Kikuu kugeukia Ulimwengu wa Nne, sio kufundisha, kwanza, bali kwa majadiliano na kujifunza. Tunapoongelea Chuo Kikuu, tunamaanisha Chuo Kikuu na taasisi zake zote na nyanja zake zote. Tunamaanisha pia Chuo Kikuu na wananchi wake wote ambao kwa namna moja au nyingine wanashikilia msimamo mmoja wa elimu.Wakati umefika wa kuridhiana kwa maarifa, yaani kusema na kuafikiana kati ya wale wote wanaojua na wale waliotengwa. Na usawa huu ni hitaji thabiti na gumu, sio suala la kuazimisha sikio la fadhili, kufanya mazoezi ya kufanana na kusikiliza, kwa njia ya tiba ya kisaikolojia. Ni suala la kuwauliza watu baki, walio chini ya ngazi ya kijamii ili kutoa hoja, mawazo yao na kile wanachokijua, kuwaomba watuchukulie kwa umakini na kutuamini. Ni lazima kueleweshana juu ya kile tunacho hitaji hapa. Tunapendekezea hii jamii au kundi lililozamishwa kwenye hofu kwa vizazi na vizazi, kuchukua hatua mpya pamoja nasi.”
Leave a comment
