Wakati huu wa Krismasi

Nilipokuwa mtoto, kutoka miaka 4 hadi 13, kila mchana baada ya shule, nilienda kwa Mchungaji Mwema ili kupata supu, mkate, mboga, wakati mwingine nyama. Watawa walitupa hii kama malipo, kwa sababu nilikuwa nikihudumia misa.

Wakati mwingine, kwa watoto wa eneo letu, nilikuwa mtoto wa supu ya “wasista wazuri”, na nilipigana wakati mama yangu alishtakiwa kutojua kupika.

Tulikuwa tukikaa katika kiwanda cha zamani kilichogawanywa kuwa vyumba kwa kutumia mbao za msonobari. Kuanzia saa kenda asubuyi wakati wa baridi na saa kumi na mbili ya asubuyi au saa moja ya asubuyu wakati wa kiangazi, mwanga ulikataa kuingia jikoni.

Ilikuwa ni makazi duni, sisi ndio wenyeji na watu hawakuthubutu kuja nyumbani kwetu isipokuwa kuleta viatu na nguo. Mama yangu alikuwa mwepesi kushukuru, hatakama hayakuitajika.

Hata hivyo, wakati huo wa maisha yangu ambapo umaskini ulikuwa mbaya sana, kuna kipindi tulifurahi kwelikweli. Ilikuwa wakati wa Krismasi. Sijui ni nani katika familia aliyeunda pango cha kwanza. Ukweli unabaki kuwa, mwaka baada ya mwaka, palikuwa pamekuwa mahali pa kukutania kukutania watoto wote wa jirani na hata wazazi wao. Kila mwaka tuliunda wahusika huko, tuliongeza pango? Sisi, ambao tulikuwa familia maskini zaidi, tulikuwa na kitu cha kumpa kila mtu ili kufanya jirani kuwa na furaha na huyo alikuwa Mungu Mwema.

Katika wakati hizi za Krismasi tulikuwa tumeweka pango katika eneo lililokuwa linaitwa “chumba ndogo”. Ilikuwa ni chumba ndogo ambacho watu walikuwa wakilala kwa kawaida, dirisha ya pekee ambalo lilifunguliwa barabarani, na wapita njia waliweza kukiona. Kwa sababu yake, tulipata heshima na tulijivunia; tulishiriki kuwafurahisha watoto, wawe matajiri au maskini. Kwa nini nilikumbuka pango hiki wakati huo wa majiko ya supu, akiba za vyakula, ziada inayoongezeka kwa ukosefu wa ajira?

Ni kwa sababu ninaamini kwamba kutokuwa na hisia kwa kuvunjiwa heshima, watoto wanaweza kuunda furaha? Wanaweza kutukumbusha sisi watu wazima tunaofanya vibaya ili kujenga amani na haki, kwamba si mambo yanayosuluhisha maafa, wala kugawana mali, bali kwamba haki inajengwa na watu ambao unyoofu wao hauwezi kutiliwa shaka? Na unyoofu huu, watoto wanayo kwa undani. Hii ndiyo sababu hawatoe maadhuru bali mfano wakati huu wa Krismasi.

0 comments Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.