Familia lazima zione fahari

Katika sehemu ya pili, Joseph Wresinski anawaambia familia maskini zaidi kuwa na fahari ndani yao kwa sababu ya moyo wa mama na baba walionao.

Fahari. Kuwa na fahari katika nafsi ni jambo la muhimu. Familia lazima zione fahari. Kina mama wanao moyo na lazima wajue hivyo.

Lazima wawe na fahari kwa jinsi wanavyolea watoto wao wakati kipato chao ni finyu. Kina baba hawana budi wajivune kwa sababu hata katika hali ya kutokuwa na fedha, hata katika hali ambayo matumbo yao huwa matupu tena wakivaa nguo zisizo na maana, lakini bado wanakwenda kazini. Ndiyo. Tena kwa fahari. Kwa fahari hii watadai kila kitu : watadai elimu, haki ya elimu kwa watoto wao, hususan wakizingatia zaidi wale walio wadogo zaidi. Kwa sababu ni kuanzia katika umri mdogo ndipo watoto hujifunza kujivunia mazingira yao halisi. Wanapaswa wafunzwe kupenda asili yao, kama jinsi wanavyojipenda wao wenyewe. Lazima wafundishwe kuwapenda rafiki zao, watu waliokua pamoja, ili kwamba kamwe wasiwasahau na kuachana na watu wa kwao.

0 comments Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.