Wakati una kimbia,
Ni wakati wa kuelewa
kuwa hakuna sherehe yoyote
ambayo si sherehe ya wote.
Ni wakati wa kutaka sherehe itukutanishe sote.
Katika usiku wa Krismasi, umeme urudishwe hatimaye
na tuweze kwa mara ya kwanza kuzima mshumaa.
Iwe ni kwamba tishio la kufukuzwa halitatusumbuwa tena
kwa sababu hatimayee deni la kodi limelipwa.
Ni wakati wakutoanza tena hofu
ya njaa katika siku za mwisho za mwezi.
Iwe kwamba makazi hayataendelea kuwa
kama zamani bila moto.
Je, wakati huu, mtu hatakuwa tena bila kazi isiyosaidiwa,
kwamba mavazi ya bure hayatawavika watoto tena,
kwamba maskini hawatakuwa na aibu ya kwenda kuomba viungo vya nyama
mwishoni mwa soko, ili kuviweka pamoja na sahani ya viazi?
Wakati una kimbia…
Je, umewadia wakati ambapo maskini hawatakuwa na hofu tena
na sherehe itakavyoishi hatimaye.
