“Ninatoa ushuhuda kwenu” uliosomwa kwa mara ya kwanza wakati wa maadhimisho ya kwanza tarehe 17 Oktoba 1987.
Ninyi mamilioni kwa mamilioni ya watoto, akina mama kwa akina baba waliofariki kwa ufukara na njaa, tuliowarithi.
Ninyi mliokuwa hai, Siyo kifo chenu ninachokitambulisha leo Kwenye Uwanja huu wa Fadhila, Wa Haki za binadamu na Raia Bali ni maisha yenu ninayoyashuhudia.
Nawashuhudia ninyi, akina mama Mnaoona watoto wenu wanahukumiwa Kuishi katika ufukara, Wakawa kama mali ya ziada duniani humu.
Nashuhudia watoto wenu Wenye mwili ulionyong’onyea kwa mateso ya njaa Waliopoteza tabasamu Bado wangalitaka kupenda.
Nashuhudia mamilioni ya Vijana Waliopoteza sababu zao za kusadiki wala za kuwepo duniani, Wakitarajia bure siku za usoni Duniani humu kusiko na maana.
Nawashuhudia maskini wa nyakati zote na tena wa leo
Wanaovutwa na safari Wakakimbia huku na kuko kati ya dharau na chuki.
Wafanyakazi, wasio na fani, Wanaotingwa muda wote na kibarua, Wafanyakazi ambao mikono yao sasa, Haina faida tena.
Mamilioni ya wanaume wanawake na watoto Ambao mioyo yao bado hupiga Mapigo makubwa ya kujitahidi, Akili zinaasi dhidi ya majaliwa yasiyo na haki Waliokandamizwa Wenye ushupavu unaodai haki ya kuthaminika zadi.
Nawashuhudia Ninyi watoto; wanawake kwa wanaume Mnaokataa kulaani, bali kupenda kusali, kufanya kazi na kushirikiana ili izaliwe ardhi yenye ushirikiano, ardhi moja, ardhi yetu, ambapo kila mtu angaliweka ndani yake wema wake uliobora kabla ajafa.
Nawashuhudia Wanaume, wanawake na watoto Ambao sifa yenu imeishachongwa Kwa moyo, mkono na chombo Katika jiwe la Uwanja huu wa Fadhila.
Nawashuhudia ili watu, mwisho Wajiongoze katika busara Wakakatalia kwa daima kule kuwa fukara hakuwezi kuepukwa.
Photo: Giovanni T – CC BY-SA 4.0