Mnamo Oktoba 17, 1987, Padre Joseph Wresinski, mwanzilishi wa ATD Dunia ya Nne, alizindua bamba kwenye jumba la Haki za Kibinadamu na Uhuru, eneo la Trocadéro huko Paris, ambapo maneno haya yamechorwa:
“Mnamo Oktoba 17, 1987, watetezi wa haki za binadamu na haki za kiraia kutoka nchi zote walikusanyika kwenye jumba huu. Walitoa pongezi kwa wahasiriwa wa njaa, ukosefu wa maarifa na vurugu. Walithibitisha imani yao kwamba umaskini si wa kuua. Walitangaza mshikamano wao na wale wanaopambana duniani kote kuuangamiza.
Popote pale wanaume kwa wanawake wanapolazimika kuishi katika maisha ya umaskini uliokithiri, haki za binadamu hukiukwa. Sote ni wajibu wetu wa dhati kujiunga pamoja na kuhakikisha kwamba haki hizi zinaheshimika. ” Padre Joseph Wresinski

Akiwahutubia watu 100,000 waliohudhuria, Padre Joseph alitoa pongezi kwa maskini wa wakati wote, kupitia hotuba yake, “Nashuhudia juu yenu.”

Maandamano haya ya Oktoba 17, 1987, yalipelekea kuundwa kwa siku ya kutokomeza umaskini uliokithiri duniani, iliyotambuliwa rasmi mwaka 1992 na Umoja wa Mataifa kama “Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini.”
